Baraza la maaskofu wa kikatoliki nchini Nigeria limezitolea wito pande zote zinazohusika ziyatambue matokeo ya uchaguzi wa bunge na rais nchini humo.Wito huo umelengwa zaidi vyama vikuu viwili vya kisiasa ambavyo wafuasi wake wametakiwa wadumishe amani"-hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Guardian la Nigeria lililomnukuu mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki,askofu mkuu wa Abuja Ignatius Kaigama.Amewasihi wanigeria wajiepushe na machafuko, matokeo rasmi yakitangazwa,ili kama alivyposema kutowapa uwanja wanamgambo wa itikadi kali wa Boko Haram kufanya mashambulio.Matokeo ya hadi sasa ya uchaguzi yanaashiria ushindi wa mgombea wa upande wa upinzani Muhammadu Buhari.Anasemekana amempita kwa kura laki tano rais anaemaliza wadhifa wake Godluck Jonathan.Mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kikatoliki nchini Nigeria,Ignatius Kaigama amewapongeza wananchi wa nchi hiyo yenye wakaazi wengi zaidi barani Afrika kwa moyo wa amani waliouonyesha katika zoezi la kupiga kura.Tume ya uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais wakati wowote kutoka sasa.Hata hivyo chama cha upinzani cha jenerali wa zamani Buhari kimeshajitangazia ushindi wanaoutaja kuwa wa kihistoria.
31 Machi 2015 - 19:41
Msimbo wa Habari: 680320
Baraza la maaskofu wa kikatoliki nchini Nigeria limezitolea wito pande zote zinazohusika ziyatambue matokeo ya uchaguzi wa bunge na rais nchini humo